Diwani wa Kata ya Isebya wilayani Mbogwe mkoa wa Geita, George Mbapula amesema atahakikisha anaisimamia Serikali katika kuendelea kuboresha huduma ya maji katika kata hiyo, ili azma ya Serikali ya kumtua Mama ndoo kichwani ifanikiwe kwa asilimia 100.
Mbapula amesema hayo baada ya kuapishwa katika Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe, kufuatia ushindi alioupata katika uchaguzi mdogo wa Madiwani uliofanyika Machi 20, 2024 katika Kata 23 za Tanzania Bara.