Dirisha la udahili TCU lafunguliwa

0
424

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imefungua dirisha la udahili kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza wanaotaka kujiunga na Taasisi za Elimu ya Juu nchini.

Katibu Mtendaji wa TCU Profesa Charles Kihampa amesema dirisha hilo limefunguliwa leo Julai 12 na litafungwa Agosti 5 mwaka huu.

Profesa Kihampa amewataka waombaji wafuatilie taarifa zaidi katika tovuti za TCU na vyuo wanavyotaka kujiunga, na kufanya maombi kwa njia ya mtandao pamoja na kuepuka usumbufu wa kutapeliwa.

Amesema TCU inatarajia kudahili waombaji zaidi ya elfu tisini ikiwa ni ongezeko zaidi ya mwaka wa masomo uliopita ambapi ilidahili waombaji 87,934.