Hadi kufikia mwezi Aprili mwaka huu deni la serikali lilikuwa shilingi trilioni 69.44.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amesema katika kipindi kama hicho mwaka 2021 deni la Serikali lilikuwa shilingi trilioni 60.72.
Amesema kumekuwa na ongezeko la asilimia 14.4 ya deni la serikali kwa mwaka 2022 tofauti na lile lililokuwa mwaka 2021.
Dkt. Nchemba alimeambia bunge jijini Dodoma kuwa kati ya kiasi hicho, deni la nje lilikuwa shilingi trilioni 47.07 na deni la ndani lilikuwa shilingi trilioni 22.37.
Amesema ongezeko la deni la Serikali lilitokana na kupokelewa kwa mikopo mipya kutoka vyanzo vyenye masharti nafuu na ya kibiashara kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo.
Waziri huyo wa Fedha na Mipango alikuwa akiwasilisha bungeni hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2021 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.