DAWASA yaadhimisha siku ya mazingira kwa kupanda miti

0
180

Na,Emmanuel Samwel

Katika kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani ,wananchi waishio karibu na miundombinu ya maji nchini wametakiwa kutambua umuhimu wa kushirikiana na wadau wa mazingira kupanda miti katika maeneo hayo ili kutatua changamoto ya upatikanaji maji safi na salama.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Idara ya Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) Mhandishi Modester Mushi wakati wa zoezi la Upandaji Miti zaidi ya elfu moja katika eneo la mtambo wa Maji Ruvu Chini Mkoani Pwani.

“Zoezi la Upandaji Miti katika kingo za mto zitasadia kulinda mmomonyoko wa udango unaoweza kusababisha kuziba kwa mabomba yanayosambaza maji katika maeneo mbalimbali” Amesema Mhandishi Mushi.

Nao baadhi ya wananchi wanaoishi katika eneo la mtambo wa maji RUVU chini wameshauri kuwepo na semina za mara kwa mara kwa wananchi juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji utakoweza kuwa na uhakika wa maji safi na salama.

Kwa upande wake Meneja Uzalishaji maji Mtambo wa Ruvu Chini Mhandishi Immaculata Msilama amesema shughuli za binadamu pembezoni mwa mto Ruvu bado ni changamoto kubwa inayohitaji ushirikiano wa pamoja kuokoa vyanzo vya maji.

Zaidi ya Miti elfu Moja imepandwa hii leo na watendaji wa DAWASA katika eneo hilo ili kuimarisha kingo za maji ya mto huo.