Dawasa kuendelea kukarabati miundombinu

0
193

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), imeendelea kuboresha huduma ya Majitaka ili kuepukana na magonjwa

Meneja usimamizi wa huduma za Maji Taka Mhandisi Joyce Mwanjee, amesema Idara ya Maji Taka kwa sasa wanatoa usajili kwa watanzania wenye magari ya kubeba maji taka ili kushirikiana kufanya kazi hiyo kwa ajili ya kuweka mkoa safi.

Naye Mkurugenzi Idara Majitaka, Mhandisi Lydia Ndibalema amesema tayari Benki ya Dunia imeshatoa ufadhili wa kuboresha miradi ya mifumo ya maji taka katika Jiji la DSM hivyo kufikia mwaka 2025 miradi mingi itakuwa imekamilika

“Pesa ipo kwa hisani ya benki ya dunia na haya ndio malengo ya DAWASA idara ya maji taka ifikapo 2025,”- amesema Mhandisi Ndibalema.

Mwaka wa fedha wa 2021/2022 unatarajiwa kukamilisha miradi hiyo itapelekea kunufaisha zaidi ya Wakazi 700 wanaokadiliwa kuwa sita au saba kwa kaya Moja

Mkaazi wa Changanyikeni Suzana Kuuzenza amesema kabla ya kutumia magari ya maji taka ya DAWASA walikuwa wanapata tabu kutoka kwa watoa huduma wengine hasa kwenye swala la muda na unafuu wa bei ya kunyonyewa maji hayo.