Dawa za asili kurasimishwa

0
201

Akihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo, Novemba 13, Rais, Dkt. John Magufuli amesema anatambua mchango wa dawa za asili katika sekta ya afya.

Magufuli amesema hayo akiainisha taswira ya mambo yanayokusudiwa kufanywa katika kuboresha na kuimarisha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi kwa kuongeza watendaji, miundombinu, vifaa tiba na vifaa kinga.

“Mbali na kumtanguliza Mwenyezi Mungu, tiba za asili au tiba mbadala nazo zimesaidia sana. Hivyo basi kwa miaka mitano ijayo, tumekusudia kuimarisha kitengo cha utafiti wa tiba mbadala.

“Sisi Watanzania hatupaswi kamwe, kudharau dawa zetu za asili au tiba mbadala. Na kwa sababu hiyo matibabu na maduka rasmi ya dawa asili yataruhusiwa,” amesema Rais Magufuli.

Kauli hii ya Rais wa Tanzania imetokana na mchango wa tiba asili katika kupambana na Virusi vya Corona (COVID-19) hapa nchini.