Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) umetangaza kuwa Daraja la Tanzanite jijini Dar es Salaam litafungwa kuanzia Januari 2 hadi Januari 9 mwaka huu.
TANROADS imesema sababu ya kifungwa ni kutoa nafasi ya kuweka nembo ya Tanzanite, hivyo, kwa muda wote huo daraja halitotumika kwa sababu za kiusalama.
Uwekaji nembo hiyo ni utekelezaji wa maelekezo aliyotoa Rais Samia Suluhu Hassan mapema mwaka jana wakati akizindua daraja hilo, ambapo alisema nembo ya Tanzanite juu ya daraja hilo itaakisi jina la daraja.
Kwa sasa juu ya daraja hilo linalokatiza juu ya Bahari ya Hindi kuna nembo ya Mwenge wa Uhuru.