Dar yatoa Ratiba ya kumuaga Dkt. Magufuli

0
204

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge ametoa ratiba na utaratibu wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Dkt. John Magufuli ambapo kwa Mkoa huo umepewa siku mbili za kutoa heshima za mwisho.

Akitoa ratiba hiyo Kunenge amesema Siku ya kesho Jumamos Machi 20 kuanzia saa 1:00 -3:00 Asubuhi itafanyika Misa takatifu kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro, Saa 3:00 – 3:30 asubuhi Mwili wa Marehemu utawasili Uwanja wa Uhuru, Saa 3:30 – 4:30 asubuhi itafanyika Misa takatifu ambapo Saa 4:30 Asubuhi adi Saa 9: 30 Alasiri Viongozi wa Serikali, Vyama vya siasa, Wafanyakazi na Taasisi za umma watatoa heshima za mwisho na majira ya saa 9:30 – 12:00 Wananchi watatoa heshima za mwisho.

Aidha Kunenge amesema Siku ya Jumapili Saa 2:00 Asubuhi mwili wa Marehemu utawasili Uwanja wa Uhuru, Saa 2:30 Asubuhi hadi Saa 10:30 Jioni Wananchi watatoa heshima za mwisho ambapo Saa 10:30 Jioni adi Saa 11:00 jioni Mwili utaelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ambapo saa 11:00 jioni hadi Saa 11:45 jioni Mwili utasafirishwa kutoka Dar es salaam kuelekea Dodoma.

Katika hatua nyingine Kunenge ametoa kibali kwa Daladala, Bajaji na Bodaboda kupeleka wananchi Uwanja wa Uhuru hatakama hawana route za kuelekea huko ili kurahisisha suala la usafiri huku akitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi.