Daladala jijini Dodoma zagoma kutoa huduma

0
184

Mabasi madogo maarufu kama daladala yanayofanya safari katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dodoma leo yameanza mgomo, ambapo madereva wa mabasi hayo wamesema wataendelea na mgomo huo hadi hapo kero zao zitakapopatiwa ufumbuzi.

Wamedai kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia ubovu wa miundombinu katika kituo cha mabasi madogo cha Sabasaba wanachotumia kuegesha magari yao, kituo ambacho pia ni kidogo.

Wakizungumza na Mwandishi wa TBC jijini Dodoma, abiria wanaotumia.mabasi hayo madogo wamelalamikia kitendo cha kusimama kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi kutokana na kuwepo kwa mgomo huo.