Daktari amefanya upasuaji Zanzibar akiwa Dar

0
337

Mbunge wa jimbo la Kawe lililopo Dar es Salaam Josephat Gwajima amehoji juu ya maandalizi ya kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya akili mnembe [artificial Intelligence] ambayo inaonekana kupoteza ajira za watu wengine.

Amesema Januari 27, 2024 yalifanyika majaribio ya mwalimu kufundisha Dodoma akiwa Kibaha – Pwani na jaribio jingine ambalo daktari alifanya upasuaji Zanzibar akiwa Dar es Salaam na upasuaji huo ukafanikiwa.

Amehoji pia kutokana na matumizi mengine kama ya roboti kufanya shughuli za binadamu, Serikali imejiandaa vipi na upotevu wa ajira kutokana na teknolojia hizo kuchukua ajira za Wananchi.

Hayo yamejiri Bungeni Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.