CT-Scan Rukwa mkombozi kwa wagonjwa

0
164

Kwa mara ya kwanza mkoani Rukwa Serikali ilinunua mashine mpya ya kisasa ya CT-Scan na tangu kufungwa kwa mashine hiyo Desemba 2022 imehudumia wagonjwa takribani 96.

Naibu katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe amesema Serikali kupitia wizara ya afya imeendelea kufanya uwekezaji mkubwa wa vifaa tiba vya kidijitali ili kuwezesha na kurahisisha upatikanaji wa huduma bora kwa Wananchi.

Mteknolojia wa Mionzi, Lutfia Khamis amesema kabla ya kununuliwa kwa mashine hiyo wagonjwa walikuwa wanaenda hospitali ya Kanda Mbeya, umbali wa kilomita 340 kupata huduma hiyo.

“Wakati nahamia hapa palikuwa na X-ray moja tena ya kianalojia na imechoka, leo siamini Rukwa kuna CT-Scan, X-ray mbili za kidijitali, yaani nafurahia kazi yangu, nimshukuru sana Rais Dkt. Samia uwekezaji huu mkubwa alioufanya katika hospitali yetu,” amesema Lutfia.