CPA Kasore ateuliwa Mkurugenzi Mkuu VETA

0
218

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua CPA Anthony Mzee Kasore kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Kabla ya uteuzi huu, Kasore alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Aidha Rais Samia amemteua Goodluck Antipas Shirima kuwa Kamishna wa Petroli na Gesi, Wizara ya Nishati.

Shirima ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Uhusiano cha kampuni ya mafuta ya Puma, Tanzania.