Corona yawakosesha watoto wengi masomo

0
355

Shirika la Kimataifa linalohudumia watoto la Save The Children limesema watoto milioni 10 katika maeneo mbalimbali duniani watashindwa kwenda shule kama walivyokuwa wamezoea, kutokana na madhara ya virusii vya corona.

Taarifa ya hivi karibuni iliyotolewa na shirika hilo imeeleza kuwa watoto wengi wanaweza kusahau kusoma na kuandika na wengine kusahau kile walichojifunza shuleni, baada ya shule nyingi kufungwa kwa muda mrefu.

Mataifa mengi yameamua kufunga shule hasa za msingi ili kuwaepusha watoto kupata maambukizi ya corona, ambayo tayari yamesababisha maafa kwa maelfu ya watu katika meneo mbalimbali duniani.

Shirika hilo la Save The Children limesema ni vema ikatafutwa elimu mbadala kwa watoto hasa kutoka katika nchi maskini ili kuwanusuru dhidi ya ujinga na elimu ambayo wangepaswa kuipata mashuleni.