Rais John Magufuli amesema kuwa idadi ya wagonjwa nchini Tanzania imepungua sana, huku baadhi ya vituo vilivyotengwa kwa ajili ya kuwahudumia wenye maambukizi vikiwa vitupu.
Rais amesema hilo wakati akitoa salamu kwa Watanzania alipohudhuria ibada ya Jumapili- KKKT Usharika wa Chato Mkoani Geita,
Akitoa takwimu hizo Rais Magufuli amesema kwa Mkoa wa Dar es Salaam;
Amana ilikuwa inalaza wagonjwa 198 leo walikuwepo watu 112 walioathirika, Mloganzila walikuwa watu 30 leo 6, Kibaha huwa wanalazwa watu zaidi ya 50 leo wamebaki watu 22 ambao hali zao ni nzuri.
Akitaja vituo vingine amesema Aga Khan wamebaki watu 31, Hindu Mandali wamebaki 16, Regency 17, TMJ wamebaki 7, Rabininsia wamebaki 14.
Katika mikoa mingine amesema, Arusha kuna vituo vitatu, Moshono kuna wagonjwa 11, Longido na Karatu hakuna mgonjwa.
Mwanza kuna vituo 10 ambapo Buswelu kuna wagonjwa 2, Misungwi 2
Ukerewe, Magu, Mkuyuni, Bachosa, Sengerema, Kwemba kote hakuna mgonjwa, huku Hospitali ya Bungando na Sékou Touré kuna wagonjwa 2 wenye uhitaji maalum.
Dodoma kuna vituo vinne ambapo mjini viko viwili kuna wagonjwa wawili
huku Kongwa na Kondoa kukiwa hakuna hakuna mgonjwa.