Mkurugenzi wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam, Tumaini Gurumo amesema chuo hicho kimetoa fursa kwa Wanawake kujifunza masomo ya ubaharia bila vikwazo.
Amesema wameamua kufanya hivyo baada ya kubaini kuwa idadi ya Mabaharia Wanawake nchini ni ndogo ikilingamishwa na katika mataifa mengine.
Gurumo ameongeza kuwa
Serikali imekuwa mstari wa mbele kupeleka chuoni hapo mitambo mbalimbali ya kisasa ambayo inasaidia katika kutoa elimu ya nadharia kwa Wanafunzi ambao wamekuwa walikimaliza masomo yao wakiwa na ujuzi stahiki.
“Tuna mpango wa kuwa na matawi Lindi, Busega – Simiyu, Pemba, Mwanza mjini Lakini pia tumepata eneo ingawa halipo kwenye maji Kigoma”. Amesema Gurumo
Ameiomba Serikali kuwaongezea majengo kwa kuwa Wanafunzi wanaongezeka hali inayosababisha kutokuwa na mazingira rafiki ya wanafunzi kusoma.
Imeandikwa na: Happyness Hans