Chuma cha Liganga kitumike kwenye viwanda

0
294

Rais Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji kuhakikisha mradi wa chuma wa Liganga unaanza uzalishaji na malighafi hiyo itumike na viwanda vya hapa nchini.

Akizindua kiwanda cha kuunganisha malori na matipa cha Satarn kilichopo Kigamboni mkoani Dar es Salaam, Rais Samia amesema malighafi zinazopatikana katika mradi wa chuma wa Liganga zitasaidia utengenezaji wa vipuri na bidhaa nyingi zinazozalishwa na viwanda vya ndani.

Rais Samia amesem mradi huo ni muhimu kwa uchumi wa viwanda vya chuma na amewataka mawaziri hao kuhakikisha wanapata mwekezaji mzuri atakayechimba chuma hicho na kisha kitumike kwenye viwanda vingine.

Kiwanda hicho cha kuunganisha magari cha Saturn ni cha pili kujengwa hapa nchini ambapo pamoja na mambo mengine kinaunganisha malori na matipa aina ya HOWO na matela yake.