Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo amewahimiza wananchi wa Mji wa Mwakitolyo wilayani Shinyanga kuimarisha ulinzi wa miundombinu ya Maji ya KASHWASA.
Chongolo ametoa rai hiyo mapema leo asubuhi kwenye mkutano wa hadhara aliofanya katika Kijiji hicho cha Mwakitolyo.
Chongolo amesisitiza kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa jamii na wananchi wote kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha miundombinu hiyo ya Maji haihujumiwi au kuharibiwa na watu wenye nia ovu kwani Serikali imetumia gharama kubwa sana kwenye miundombinu hiyo.
Awali, Chongolo ameipongeza KASHWASA kwa kazi nzuri iliyoifanya kwenye ujenzi wa Tangi hilo la Maji. Pia ameridhishwa na ubora wa ujenzi wa Tangi hilo.
Chongolo amesema kwamba kukamilika kwa ujenzi wa Tangi hilo kunaenda kuchochea shughuli za kiuchumi hususani kwenye sekta ya madini ambayo ndo shughuli kubwa ya wakazi wengi wa Mwakitolyo.