CHONGOLO: Imarisheni mashina ya CCM

0
211

Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Daniel Chongolo amewataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kuimarisha uwepo wa mashina ikiwa ni pamoja na kufanya mikutano iliyopo kikatiba.

Chongolo ametoa kauli hiyo wakati alipokua akizungumza na wanachama wa shina namba sita tawi la Zizini B, Handeni mkoani Tanga.

Amesema uhai wa chama upo kuanzia ngazi ya shina kwa kuwa huko ndipo walipo wanachama hivyo ni vema kila mmoja akatimiza wajibu wake wakiwemo wanachama na viongozi.

Aidha, Chongolo amesema CCM kitaendelea kusimamia vema utekelezaji wa ilani ikiwa ni pamoja na kuwaletea maendeleo wananchi kwenye maeneo yao.