Chongolo amtaka waziri Babati

0
206

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo, amemtaka Waziri wa Maliasili na Utalii kwenda Babati mkoani Manyara na kukutana na wakazi wa vijiji tisa kuangalia namna ya kumaliza mgogoro wa mipaka baina ya hifadhi ya Tarangire na vijiji hivyo vilivyopo pembezoni mwa hifadhi hiyo.

Chongolo amesema hayo alipolakiwa na wakazi wa vijiji vya kata ya Magara ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani Manyara, yenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wananchi.

Chongolo amesema Wakazi hao wana haki ya kufahamu zaidi ukweli kuhusu mgogoro huo pamoja na hatma yao.