Chongolo alia na miiko ya uongozi

0
206

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo ambaye anaendelea na ziara yake ya siku tisa mkoani Morogoro, leo ameanza ziara yake wilayani Mvomero.

Akiwa wilayani humo, Chongolo amewataka viongozi wa wilaya hiyo kuzingatia miiko ya uongozi hasa wakati wanatatua migogoro ya wakulima na wafugaji.

Amesema hatua ya viongozi hao kutekeleza majukumu yao pasipo kuzingatia miiko ya uongozi ni moja ya chanzo cha kuibuka kwa migogoro mingi ya ardhi.