Chongolo aeleza alivyokagua sekta ya elimu Morogoro

0
147

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo amehitimisha ziara yake ya siku tisa mkoani Morogoro ambapo pamoja na mambo mengine
amekagua miundombinu katika sekta ya elimu.

Amesema akiwa mkoani humo ameangalia mgawanyo wa idadi ya walimu kwa msawazisho wa kila wilaya na kubaini mapungufu kwenye msawazisho wa walimu na hivyo kumtaka Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu David Silinde kueleza wamejipanga vipi kurekebisha mapungufu hayo.

Chongolo amesema pia ameangalia mgawanyo wa vishikwambi kwa walimu na kujiridhisha walimu wote wa mkoa wa morogoro wamepata Vishikwambi hivyo.

Kuhusu utoaji elimu bila malipo Chongolo amesema amekagua ikiwa fedha za kufidia elimu hiyo zinafika kwenye shule za mkoa wa Morogoro.

Katika ziara yake ya siku tisa mkoani Morogoro, Katibu Mkuu huyo wa CCM Taifa amezitembelea wilaya zote 7 za mkoa huo pamoja na halmashauri zake 9.