Charles Hilary Mkurugenzi mpya wa Idara ya Mawasiliano Ikulu

0
236

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amemteua Charles Martin Hilary kuwa Mkurugenzi wa Idara ya mawasiliano Ikulu Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar imeeleza kuwa Dkt. Mwinyi pia amemteua Yusuph Majid Nassor kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) na Dkt. Idrissa Muslim Hija kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uhaulishaji Ardhi Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi huo umeanza leo.