Chanzo cha moto Mlima Kilimanjaro chatajwa

0
104

Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) William Mwakilema amesema, kamati ya kuchunguza chanzo cha moto katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro imebaini kuwa moto huo uliokuwa ukiwaka katika hifadhi hiyo ulisababishwa na shughuli za kibinadamu.

Akitoa taarifa ya kamati hiyo mbele ya waandishi wa habari jijini Arusha Mwakilema amesema, jeshi la uhifadhi limekuwa na mikakati ya kukabiliana na changamoto ya mioto katika hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, mikakati iliyowezesha kuuzima moto huo licha ya changamoto mbalimbali zilizojitokeza.

Ameongeza kuwa moto huo umekuwa na madhara ikiwa ni pamoja na kuteketeza eneo la miti inayosaidia ekolojia ya mlima Kilimanjaro.