Chanjo ya UVIKO19 ruksa kwa vijana kuanzia miaka 18

0
397

Kutokana na uhitaji wa chanjo kwa Watanzania wengi, serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza ruksa kwa yeyote anayefika kwenye kituo cha afya kwa ajili ya huduma ya chanjo achanjwe.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima ameyasema hayo wakati wa mdahalo maalum mkoani Dar es Salaam ambapo ameainisha kuwa mpaka kufikia Agosti 8, 2021 zaidi watu wapatao 100,000 walikuwa wameshachanjwa.

“Baada ya kupata ratiba ya ujio wa chanjo nyingine na kwa ushirikiano mzuri wa serikali yetu, wadau wametoa ratiba yao hivyo tumeona tupanue wigo wa makundi,” amesema Dkt. Gwajima.

Kwa upande wa Mbunge Neema Lukangira ambaye ameshiriki kwenye mdahalo huo amesema kuwa ni nafasi kwa bunge kuwa sehemu ya historia kwa kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanikiaha zoezi la chanjo.

Zoezi la chanjo lilizinduliwa rasmi Julai 28, 2021 na Rais Samia Suluhu Hassan ambapo yeye na viongozi wengine walichanjwa.