Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sity Nyahoza amesema kuwa sheria ya uchaguzi inazuia chama cha siasa kutumia zaidi ya shilingi bilioni 17 kwa mchakato mzima wa uchaguzi, na chama kitakachokiuka kitapewa adhabu ikiwa ni pamoja na kufutiwa matokeo hata kama kimeshinda.
Akizungumzia suala la vyama vya siasa kupokea fedha kutoka nje kwa ajili ya uchaguzi, amesema muda huo kwa sasa umekwisha kwa sababu chama kinatakiwa kupokea fedha siku 90 kabla ya uchaguzi.
Msikilize hapa chini akitolea ufafanuzi hoja hizo;