Chama Cha Mapinduzi kuzindua kampeni Zanzibar leo

0
399

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatarajiwa kuzindua kampeni zake za kusaka urais wa Zanzibar leo, shughuli itakayoongozwa na na Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein.

Katika uzinduzi huo utakaofanyika Uwanja wa Demokrasia (Kibandamaiti), mgombea wa CCM, Dkt. Hussein Ali Mwinyi atatangaza ilani ya chama hicho kwa wananchi kwa kueleza mambo atakayoyafanya endapo atachaguliwa kushika wadhifa huo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu.

CCM imewataka wanachama, wafuasi wa chama hicho na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kuweza kumsikiliza mgombea huyo ili kufanya maamuzi sahihi siku ya uchaguzi.

Baada ya uzinduzi huo mgombea huyo atazunguka katika maeneo mbalimbali visiwani humo akinadi sera za chama na kuomba ridhaa ya wananchi kuongoza Taifa hilo.