CHADEMA yakoshwa na mwenendo wa maridhiano

0
165

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeeleza kuridhishwa na mwenendo wa mazungumzo ya maridhiano na hatua ambazo zimechukuliwa mpaka sasa, na kuitaka timu ya mazungumzo iendelee nayo.

Uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha dharura cha Kamati Kuu ya CHADEMA iliyokutana Januari 5, 2023 ambapo ilijadili taarifa na mwenendo wa mazungumzo hayo baina ya CHADEMA na CCM/Serikali.

Aidha, kufuatia Rais Samia Suluhu Hassan kuondoa zuio kwa mikutano wa hadhara, kamati hiyo imetangaza uzinduzi rasmi wa mikutano ya hadhara kitaifa utafanyika Januari 21, 2023, na kisha mikutano itaendelea katika ngazi za chini za chama.

Timu ya CHADEMA katika mazungumzo inaongozwa na mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe, huku timu ya CCM ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti (Bara) Abdulrahman Kinana.