CCT yahimizwa utunzaji mazingira

0
239

Jumuiya ya Kikiristo Tanzania (CCT) mkoa wa Ruvuma imesema itaendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha suala la utunzaji wa mazingira linaendelea kusimamia kwa nguvu zote ili kuepusha athari zitokanazo na mabadiliko ya Tabianchi.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa CCT kwa mkoa wa Ruvuma Askofu Raphael Haule kutoka Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma, wakati wa Ibada ya  Ijumaa Kuu  kitaifa katika kanisa la Upendo wa Kristo Masihi lililopo Kiuma Wilaya Tunduru mkoani Ruvuma.

“Kanisa lina wajibu wa kuwakumbusha waumini wake kutunza mazingira kama Mungu alivyoagiza, sisi tunaendelea kuhimiza wajibu wa kutunza mazingira ni wa kila mtu” Amesisitiza Askofu Haule

Kuhusu suala la elimu, Askofu huyo amesema CCT ipo kwenye mpango wa kuanzisha Chuo Kikuu, hivyo kuiomba Serikali kuendelea kushirikiana vema na Kanisa ili kuhakikisha watoto wa Kitanzania walio wengi wanapata elimu ya juu.