CCM yawasilisha maoni demokrasia ya vyama vingi

0
197

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amewasilisha maoni na mapendekezo ya chama hicho kwa Kikosi Kazi cha Rais Samia Suluhu Hassan kinachofanyia kazi masuala yanayohusu demokrasia ya vyama vingi vy siasa.

Katika kikao hicho cha kuwasilisha maoni na mapendekezo ya Chama Cha Mapinduzi kilichofanyika mkoani Dar es Salaam, Chongolo aliongozana na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Unenezi Shaka Hamdu Shaka.