Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa tathmini ya mwenendo wa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge katika majimbo ya Muhambwe na Buhigwe mkoani Kigoma.
Akitoa tathmini hiyo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka amesema kampeni hizo zinaendelea vizuri na wagombea kupitia chama hicho wamenadi na kutangaza sera na Ilani ya CCM.
Jimbo la Muhambwe linafanya uchaguzi mdogo wa ubunge kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Mhandisi Atashasta Nditiye na jimbo la Buhigwe linafanya uchaguzi mdogo wa ubunge kufuatia Dkt. Philip Mpango kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais.