CCM yamlilia Mrema

0
124

Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa huzuni na mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha mwanasiasa mkongwe ambaye pia alikua Mwenyekiti wa Chama cha TLP Augustino Lyatonga Mrema kilichotokea leo Jumapili Agosti 21, 2022, Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemtaja Mzee Augustino Mrema kama mwanasiasa mzalendo na aliyefanya siasa za mageuzi kwa kutanguliza mbele maslahi ya Taifa.

“Nimesikitishwa na kifo cha Mwenyekiti wa Chama cha TLP Augustino Mrema. Nitamkumbuka kwa mchango wake katika mageuzi ya siasa, uzalendo na upendo kwa watanzania.” Amesema Rais Samia Suluhu Hassan

Wakati wa uhai wake akiwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi Mzee Mrema alikuwa Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini 1985-1995 na baadae kuteuliwa kushika nafasi za Waziri wa Maendeleo ya Vijana na Ajira, Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri.