Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Shaka Hamdu Shaka amesema chama hicho kinajivunia mabadiliko makubwa yaliyofikiwa Zanzibar katika kipindi cha miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ambayo yamewafanya wananchi kujiamini na kujitegemea kimaendeleo.
“Katika kipindi cha miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu licha ya kuleta ukombozi kamili, pia yamewafanya wananachi kuwa na fikra huru na kujitawala,” ameongeza Shaka.
Amesema kabla ya Mapinduzi kulikuwa na tabaka lililokuwa likikandamiza, kubagua na kuwapuuza wengine huku wananchi wakikosa haki za msingi na kutotumia fursa za kiuchumi sawa na utu wao kutothaminiwa na kuuzwa.
Januari 12 kila mwaka Wananchi wa Zanzibar huadhimisha kumbukizi ya mapinduzi wakiwakumbuka na kuwaenzi mashujaa mbalimbali waliopamba kupata kuondoa utawala wa Sultan.