CCM kuchagua Mwenyekiti Taifa

0
125

Chama cha Mapinduzi (CCM) kinatarajia kuchagua Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, wakati wa mkutano mkuu wa 10 utakaofanyika mkoani Dodoma kwa muda wa siku mbili kuanzia hapo kesho.

Mwenyekiti wa CCM Taifa atayechaguliwa wakati wa mkutano huo atahudumu kwa kipindi cha miaka mitano, huku Mwenyekiti wa sasa wa chama hicho Dkt. Samia Suluhu Hassan akitetea nafasi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dodoma, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka amesema wajumbe wa mkutano mkuu wa 10 wa CCM pia watawachagua Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar.

Shaka amesema majina ya wagombea waliopendekezwa ni Abdulrahman Kinana kwa upande wa Bara na Dkt. Hussein Mwinyi ambaye ni Rais wa Zanzibar kwa upande wa Zanzibar.