Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Charles Kichere amesema,
Taasisi 21 za Serikali, mashirika ya umma 11 na Mamlaka za Serikali za mitaa 71 zimefanya manunuzi ya shilingi Bilioni 25.95 bila risiti za kielektroniki (EFD).
Akiwasilisha kwa Rais Samia Suluhu Hassan ripoti ya ofisi ya CAG kwa mwaka 2021/2022, Kichere amesema hali hiyo imedhoofisha juhudi za Serikali katika ukusanyaji wa mapato ambayo yangetumika kwenye shughuli za maendeleo.