Butiku : Nyerere hakuamini katika kuchuma mali

0
356

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF) Joseph Butiku amesema Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere hakua mtu wa kujilimbikizia mali, bali alikuwa ni mtu ayetumia muda mwingi kujenga misingi ya uongozi wa Taifa.

Akielezea namna alivyofanya kazi na Mwalimu, Butiku ambaye amehudumu kama Katibu wa Mwalimu kwa zaidi ya miaka 20, amesema kuwa Mwalimu Nyerere hakuwa na mali yoyote na alitumia muda mwingi kujenga Taifa la watu wake.

Butiku amesema Mwalimu aliamini katika usawa na upendo na ndio maana alitumia muda wake mwingi kusimamia maslahi ya Watanzania na hakua na muda wa kutafuta mali ama kuzimiliki.

Amewataka Watanzania kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa vitendo kwa kukataa rushwa na kipiga vita umasikini, pamoja na kusimamia falsafa ya uongozi ambayo Mwalimu Nyerere alitumia muda wake mwingi kuitengeneza.

Awali akuzungumza katika Kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa, Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Mzee Paul Kimiti amesema, haridhishwi na mandhari ya eneo la Butiama na kutoa wito kwa Serikali kuona umuhimu wa kuboresha maeneo yanayozunguka wilaya hiyo.