Bunge lapitisha muswada wa sheria ya usimamizi wa maafa

0
272

Bunge limepitisha muswada wa mabadiliko ya sheria ya usimamizi wa maafa, ambapo serikali imependekeza kubadilishwa kwa ibara ya 34 ya sheria hiyo na pia kufutwa fungu la 242 katika sheria ya awali.

Akisoma mabadiliko ya sheria hiyo bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, George Simbachawene amesema, lengo la mabadiliko ya sheria hiyo ni kuongeza usimamizi katika kukabiliana na maafa.

Amesema sheria hiyo pia itaruhusu kuanzishwa kwa mfuko wa maafa, ambao utawekewa utaratibu wa kuhudumia wananchi wakati wa maafa.

Akichangia muswada huo, Mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu amesema pamoja na kuweka mpango wa usimamizi wa maafa, lakini sheria hiyo itafanya serikali iwe na uwajibikaji wa moja kwa moja wakati wa maafa.