Bunge kuendelea hadi Juni 19

0
309

Spika wa Bunge Job Ndugai amemtaka Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Freeman Mbowe kufuata taratibu za Kibunge katika kuikosoa serikali badala ya kuzungumza akiwa nje ya bunge.

Spika Ndugai ameeleza hayo Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akitoa taarifa ya kusogezwa mbele kwa ratiba ya shughuli za bunge.

Amesema anasikitishwa na namna ambavyo kiongozi huyo amekuwa hatumii njia sahihi za kuikosoa serikali kwa kuzungumza zaidi kwenye vyombo vya habari badala ya kuzungumzia bungeni.

Kuhusu shughuli za bunge, Spika Ndugai amesema zitaendelea hadi Juni 19 mwaka huu badala ya Mei 28 mwaka huu, tarehe iliyotangazwa awali kuwa bunge la 11 lingevunjwa.