Mkutano wa pili wa Bunge la 12 unatarajiwa kuanza Februari 2 hadi Februari 12 mwaka huu jijini Dodoma.
Taarifa ya Ofisi ya Bunge imeeleza kuwa katika mkutano huo shughuli zitakazofanyika ni pamoja na maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu yanayotarajiwa kuulizwa na wabunge.
Pia, wabunge watapata fursa ya kujadili hotuba ya Rais ya ufunguzi rasmi wa Bunge la 12 na kujadili na kushauri kuhusu mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2021/2022.