Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na wenzake watatu, wamefutiwa mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakabili katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi iliyopo mkoani Dar es Salaam.
Mbowe na wenzake wameachiwa huru baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuwasilisha hati mahakamani hapo ya kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri lililokuwa likiwakabili.