Boti ya mizigo yazama Kigoma

0
388

Boti ya mizigo iliyokuwa ikisafiri kutoka mkoani Kigoma kuelekea Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) imeripotiwa kuzama katika ziwa Tanganyika.

Kamanda wa Polisi wa Moa wa Kigoma, James Manyama amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika Kijiji cha Karago wilayani Uvinza na kusema kuwa tayari vikosi vya uokoaji  hivi sasa viko katika eneo la tukio.