Bongo FM ni ya vijana wa Ngorongoro

0
319

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amewaambia wakazi wa Ngorongoro mkoani Arusha kuwa redio ya Bongo FM ipo kwa ajili ya vijana na mahitaji yao.

“Pia tunazindua kituo kwa ajili ya Bongo FM, tumewalenga vijana. Kule ukienda ni mambo ya vijana masaa 24 siku 7 za wiki, kwa hiyo vijana hamjaachwa nyuma tunataka twende na wakati tuhakikishe tunawahabarisha, kuwaburudisha na kuwahamasisha kufanya majukumu yenu”. amesema Waziri Nape

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kituo cha kurushia matangazo ya TBC Taifa na Bongo FM (Loliondo Ngorongoro) kwenye kiwanja cha Kassim Majaliwa Majaliwa ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko.