Bodi TARURA yaridhishwa Ujenzi wa Barabara Kilolo

0
208

Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi Mhandisi Florian Kabaka wamekagua Ujenzi wa Barabara ya Kidabaga – Boma Ng’ombe wilayani Kilolo, Iringa na kuridhishwa na ujenzi.

Akiwa Wilayani Kilolo katika ziara ya Ukaguzi wa Mradi wa Barabara za “Agri-Connect “, Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhandisi Florian Kabaka ameeleza kuridhisbwa na ujenzi wa Barabara ya Kidabaga -Boma la n g’ombe iliyojengwa kwa kiwango cha lamii yenye utefu wa km 18.3

Mhandisi Kabaka amebainisha kuwa lengo la Serikali kupitia TARURA nikuhakikisha barabara za Vijijini zinaboreshwa ili kuwezesha wananchi kusafirisha mazao yao kwa urahisi na kukuza uchumi wao.

”Tumekagua mradi huu hapa Kilolo na kujjionea kazi nzuri iliyofanywa na TARURA, mradi umekamilika na sasa wananchi watatumia muda mfupi kusafiri na kusafirisha mazao yao,” alisema Mhandisi Kabaka.

Kwaupande wake Makamau Mweyekiti wa Bodi hiyo Bibi Julieth Magambo amesema kuwa Uchumi wa wananchi unategemea Barabara na hivyo Serikali itaendelea kuboresha barabara za Vijijini ili wananchi waweze kuzifikia buduma za Kijamnii kwa urahisi na kuboresha uchumi wao.

Aidha alieleza kuwa ni jukumu la bodi kuzisimamia barabara hizo na kumuunga mkono Rais Samia ambaye ameamua kwa dhati kuhakikisha kuwa barabara za Vijijini zinafunguka na kuwafikia wananchi ili ziwaunganishe na miji na kurahisisha usafiri na usafirishaji.

Naye Mkurugenzi wa Barabara TARURA, Mhandisi Venant Komba amesema kuwa TARURA inaendelea na ujenzi wa Barabara ikiwa ni pamoja na kufungua barabara mpya ili kuwezesha wananchi kuyafikia maeneo haliyokuwa hayafikiki.

Mkoa wa Iringa ni miongoni mwa Mikoa miwili inayotekeleza miradi ya ujenzi wa barabara za Lami “ Agri-Connect “ chini ya ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Jumuiya ya Ulaya.

Mradi huu unalenga kuwasaidia Wakulima vijijini kuimarisha Mnyororo wa thamani ya Mazao yao hasa mazao ya Chai,Kahawa,Mbogamboga na mazao mengine yanayohitaji kusafirishwa kwa haraka toka Mashambani hadi Viwandani na Sokoni.