Biteko: Mimi mfuatiliaji mzuri wa TBC2, Safari Channel

0
214

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema anafuatilia sana vipindi vinavyorushwa na Shirika la Utangazaji (TBC) kupitia idhaa zake mbalimbali.

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kituo cha kurushia matangazo ya TBC Taifa na Bongo FM (Loliondo Ngorongoro) kwenye Kiwanja cha Kassim Majaliwa Majaliwa.

Pia ameipongeza TBC kwa maboresho makubwa ya miundombinu ya utangazaji, maboresho ya studio, mitambo na vifaa vya kisasa, ubora wa maudhui pamoja na ubunifu katika kuwahabarisha Watanzania.

“Mimi nafuatilia habari za TBC. Nafahamu chaneli ya TBC mahsusi kwa ajili kutangaza utalii (Safari Channel), redio ya vijana ya Bongo FM na televisheni ya vijana ya TBC2. TBC imekuwa na kampeni maalumu kama vile 27 ya Kijani kupitia Jambo Tanzania, Elimu kwa umma kuhusu Tume ya Haki Jinai, vipindi vya kimkakati vyenye lengo la kukuza uzalendo (Mizani, Jioni Njema, Jamvi la Machweo na Lulu za Kiswahili),” amesema Dkt. Biteko.

Sponsored by @ucsaftz