Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko leo Machi 31,2024 amefika kijijini Komaswa, wilayani Tarime mkoani Mara ili kuhani msiba wa aliyekuwa Askofu wa New Life Gospel Community Church (NLGCC) Jimbo la Mara Kaskazini Fransisca Gachuma ambaye alikuwa mwenza wa Christopher Gachuma, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ( NEC) Taifa kutokea Mkoa wa Mara.
Dkt. Doto Biteko amefika nyumbani kwa Gachuma akiwa ameongozana na mke wake Bernadetha Biteko.