Bilioni 6 kutatua changamoto ya maji Songwe

0
159

Na Aines Thobias, Songwe

Mbunge wa jimbo la Songwe mkoani Songwe amesema katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali inatarajia kutenga zaidi ya shilingi bilioni 6 ili kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji wilayani

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Mkwajuni, Philipo Mulugo amesema fedha hizo zitasaidia kuchochea maendeleo kwa sababu muda mwingi waliokuwa wanautumia wananchi kutafutia maji sasa utatumika kwenye maendeleo

Amewaeleza wananchi juu ya dhamira ya serikali ya kuboresha miundombinu ya barabara, elimu, afya, pamoja na kuweka mazingira mazuri ya biashara kwa wafanyabiashara wadogo, wakati na wa juu.

Kuhusu changamoto ya upatikanaji wa umeme Mulugo amesema tayari serikali imeshampeleka mkandarasi ambaye amekabidhiwa kazi ili kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika unaotosheleza mhitaji ya wananchi hususani wenye viwanda.

Aidha, Mulugo ametumia mkutano huo kutoa wito kwa wananchi wa wilaya Songwe kununua ardhi na kuwekeza kwenye madini kwa ajili ya manufaa yao na familia zao