Bilioni 4.9 zakamilisha ujenzi wa jengo la Zimamoto

0
259

Shilingi Bilioni 4.9 zimetumika katika ujenzi wa jengo la kituo kikuu cha Zimamoto na Uokoaji mkoani Dar es Salaam.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo hilo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji John Masunda ameishukuru Serikali kwa kuendelea kulisaidia jeshi hilo katika kuboresha maslahi ya Watendaji pamoja na vitendea kazi.

Amesema Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeendelea na ujenzi wa vituo mbalimbali na kutoa mafunzo kwa maafisa wake, ambapo hivi karibuni askari 27 wamepatiwa mafunzo ya uokoaji wa kwenye maji.