BILIONI 4.2 KUJENGA ‘AMBULANCE’ YA MAJINI

0
228

Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imetia saini mkataba wa ujenzi wa boti yenye vifaa vya matibabu (Ambulance Boat) ambao umesainiwa baina ya TASAC na Kampuni ya LOCA Muhendislik Gemi Mak. PLas Ve Gd. San Tic Itd Sti ya nchini Uturuki kwa kiasi cha shilingi bilioni 4.2 na utatekelezwa kwa muda wa miezi 12.

Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile amesema boti hiyo itakuwa na vifaa vyote vya kisasa kwa ajili ya matibabu ya waliopata ajali majini, kasi yake ni 30 KM/HR na inaweza kwenda umbali wa kilomita 278.

“Nimeshuhudia utiaji saini wa kuanza kujenga hospitali inayotembea majini, ujenzi wake ambao unafanyika Ziwa Victoria, Mwanza utakamilika baada ya miezi 12, wito wangu kwa Mkandarasi na TASAC ni kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati na viwango,” amesema.