Jumla ya Shilingi Bilini 28 zimepatikana kutokana mapato ya ndege mpya zilizoaingizwa nchini kuanzia mwaka 2016.
Hayo yamesemwa na Rais John Magufuli katika hafla ya kupokea ndege mpya Air Bus 220 inayotokea nchini Canada ambapo ameeleza kuwa mapato hayo yaliyopatikana ni chachu kubwa ya kufanyika kwa maendeleo zaidi katika sekta ya uchukuzi hapa nchini.
Rais Magufuli amesema anafurahi kuwa mpaka sasa Shirika la Ndege nchini limewepa kupata mapato makubwa tangu ndege hizo zimeanza kufanya kazi nchini na kulitaka kuhakikisha wanaongeza juhudi za kufanya biashara ili kuongeza mapato zaidi.
Amesema kuwa sekta ya uchukuzi inachochea sana katika suala la utalii hapa nchini na kuongeza mapato kutokana na watalii wanaokuja nchini .
Hata hivyo amewataka wafanyakazi wa ATCL kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii na kuweka uzalendo mbele na kutoa huduma zilizo bora.
Kwa mujibu wa Rais Magufuli,Tanzania ndio nchi ya kwanza kununua ndege ya aina hii katika Bara la Africa.