Bilioni 27.7 zajenga barabara Simiyu

0
219

Katika kipindi cha miaka miwili ya Rais Samia Suluhu Hassan madarakani mkoa wa Simiyu umepokea zaidi ya shilingi Bilioni 27.7 kwa ajili kujenga na kukarabati barabara zenye urefu wa kilomita 925.

Mkoa huo pia umejenga na kukarabati madaraja 13 likiwemo daraja kubwa la Itembe lililogharimu shilingi Bilioni 8.4.

Menaja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Simiyu Mhandisi John Mkumbo amesema, fedha hizo zimetolewa ndani ya miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Mhandisi Mkumbo amesema daraja la Itembe linalounganisha barabara ya Lalago – Sibiti limegharimu shilingi Bilioni 8.4 huku madaraja mengine 13 yakigharimu shilingi Bilioni 3.1.

Ameongeza kuwa fedha nyingine zimetumika kukarabati barabara kuu ya Mwigumbi – Lamadi yenye urefu wa kilomita 171.