Bilioni 23 kujenga wodi za watoto njiti

0
134

Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 23 kwa ajili ya kujenga wodi za kuhudumia watoto njiti, kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.

Naibu waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel ametoa kauli hiyo bungeni jiiini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Ritha Kabati aliyetaka kujua hatua zilizochukuliwa na serikali kukabiliana na vifo vya watoto njiti.

Naibu waziri Mollel amesema, kwa sasa serikali imeanza ujenzi wa wodi kwa ajili ya kusaidia kuhudumia akina mama wanaojifungua na kuwa na usaidizi wa karibu, hasa wanapojifungua watoto njiti.